
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya
Ufaransa, Paul Pogba amewasili katika viunga vya Calinton kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo vya afya na kabla hawajafanya makubaliano ya maslahi ya
mkataba wake na klabu.
Pogba aliuzwa mwaka 2012 kwa pauni 1.5mil kwa mabingwa wa
ligi ya Italia, klabu ya Juve, lakini anatarajia kurudi Trafford kwa kitita cha
pauni 89m ikiwa ni sawa na Euro 105mil
Pogba anatarajiwa kuvunja rekodi ya ada yake ya uhamisho,
ambapo kabla yake, rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na mchezaji wa Real Madrid
Gareth Bale aliyesajiliwa toka klabu ya Totenham ya Wingereza kwa pauni 85mil.
Pogba aliondoka Old Trafford baada ya kushindwana na
aliyekuwa kocha wake Sir Alex Fugerson kutokumhakikishia namba, na wakala wa
Pogba Mino Raiola akamtafutia klabu mpaka leo anarudi ManU kama malaika kwa
gharama ya juu Zaidi.
Siku za nyuma, kocha wa klabu hiyo alipoulizwa juu ya ujio wa
Pogba, alisema bado alikuwa hayuko tayari kuzungumzia wachezaji wa timu
nyingine, lakini baada ya mchezo wa jana wa ngao ya hisani MaU kuifunga
Leicester goli 2-1, Morinho akaibuka na kusema nilikuwa nasubiri mchezo huu
uishe, na bila shaka kesho [leo] Pogba atakuja kufanya vipimo vya afya.
Post a Comment