
Uongozi wa wekundu wa msimbazi Simba na benchi la ufundi, kwa pamoja
unawashukuru sana wanachama, washabiki wake na watu wote waliohudhuria kwenye
sherehe za miaka 80 ya klabu yetu ambazo zilijumuisha kilele cha wiki ya Simba
Day ambazo zilifanyika Jumatatu tarehe 8-8-2016 katika uwanja wa Taifa.
Pia uongozi
wa Simba unawashukuru sana kwa ushangiliaji wenu wa ‘NGUVU’ uliochagiza ushindi
mijarabu wa magoli 4-0 dhidi ya timu kongwe kutoka Kenya AFC Leopards.
Washabiki
wetu mmeonesha tofauti kubwa baina yao na sisi, kuujaza uwanja kiasi kile kwa
viingilio vyenu wenyewe na sio kuingizwa ‘BURE’ ilhali timu imetoka katika
msimu ambao haukuwa na matokeo ya kuridhisha sana ni ishara kuwa mna mapenzi
makubwa sana na klabu yenu na uongozi unaamini hilo ni deni kubwa linalopaswa kulipwa
kwa kuwapa furaha katika msimu huu wa ligi 2016/17.
Nitumie fursa
hii pia kuwakumbusha wale wanaotubeza, eti Leopards inashika nafasi za chini
kwenye ligi kuu ya Kenya na ndio maana tukawafunga 4-0. Wajiulize wao Medeama
waliowapiga ‘thalatha’ wanashika nafasi ya ngapi kwenye ligi yao wakati
wanawapa kile kisago cha mbwa mwizi?
Kimsingi timu
mwalikwa kwenye tamasha la Simba Day lazima iwe inacheza ligi kuu ya kwao na
iwe timu yenye historia iliyotukuka katika soka…AFC Leopards ni timu iliopo
katika ligi kuu nchini Kenya na historia yake kwenye soka la Afrika huwezi
kuilinganisha hata kidogo na Medeama ambayo iliwadhalilisha ‘WAKODISHWAJI’.
Mwisho
niwafahamishe kuwa timu yenu itaendelea na mazoezi kesho Jumatano pale Police
Kilwa road na weekend hii itaingia kambini tayari kwa mchezo wa kwanza wa ligi
kuu inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Imetolewa na
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SPORTS CLUB.
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SPORTS CLUB.
SIMBA NGUVU
MOJA
Post a Comment