
Ligi kuu ya EPL
imefunguliwa rasmi baada ya mchezo wa mabingwa wa ligi hiyo klabu ya Leicester
City, The Fox kucheza na mabingwa wa kombe la FA klabu ya Manchester United
mchezo uliofanyika katika dimba la Wembley na klabu ya Manchester kuibuka na
ushindi wa goli 2-1.
Mchezo huo ukifahamika
kama kombe la ngao ya hisani au kwa majina ya kizungu ukiitwa, Commubity Sheald
Cup, ulianza mnamo saa kumi na mbili za jioni kwa majira ya saa za Africa ya
mashariki ambapo Manchester chini ya mwalimu Jose Morinho wameibuka na ushindi
na hivyo kuongeza idadi ya vikombe katika hazina yao.
Klabu ya Manchester
United ilikuwa imechukua kombe hili mara 20 kabla ya mchezo huu na hivyo
kuongeza idadi na kuwa mara 21 huku ikiwa ni klabu pekee iliyochukua kombe hilo
kuliko klabu yeyote ile.
Kwa upamde wa klabu ya
Leicester, wao ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kucheza fainali hii baada ya
kuwa mabingwa wa EPL msimu ulioisha.
Mchezo ulikuwa ni wa
kuviziana sana na mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, Manchester walikuwa
wanaongoza kwa ushindi wa goli moja na kipindi cha pili kilivyoanza,
Mshambuliaji wa Leicester, Jarmie Vardy aliisawazishia timu yake na Ibrahimovic
akaweka kambani goli la pili goli la ushindi.
Kwa mchezo huo, sasa ligi
kuu ya EPL imefunguliwa rasmi na mechi zitaanza wikiendi ijao.
Post a Comment