SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: AJIBU, KICHUYA NA MAVUGO WAINOGESHA SIMBA DAY.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha na Bin Zubery Klabu ya wekundu wa msimbazi, Simba, leo imeadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwa klabu hiyo na kucheza mchezo wa ki...
Picha na Bin Zubery

Klabu ya wekundu wa msimbazi, Simba, leo imeadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwa klabu hiyo na kucheza mchezo wa kirafiki ulioitwa jina la Simba day dhidi ya klabu ya kutoka Kenya mabingwa wa zamani, timu ya AFC Leopards na klabu ya Simba kuibuka na ushindi mujarabu wa goli 4-0.

Shukrani kwa magoli ya Ibrahimu Ajibu aliyefunga magoli mawili, Shiza Kichuya pamoja na Laudit Mavugo wote wakiwa wamesajiliwa msimu huu.

Kocha wa wekundu wa msimbazi Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, alijaribu kuwachezesha wachezaji wote, lakini kiu kubwa ya mashabiki wa klabu hiyo ilikuwa ni kutaka kumwona mchezaji wa Burundi aliyekosa nafasi katika klabu ya Toulouse ya nchini Ufaransa na kusajiliwa na wekundu hao wa msimbazi ambapo,

 Mavugo nae akawadhihirishia mashabiki pamoja na uomgozi wa klabu hiyo kwamba hawakufanya makossa kumsajili baada ya kufunga goli moja na kutengeneza nafasi moja ya goli alilolifunga Shiza Kichuya.

Kiujumla mechi ilikuwa ni ya kuvutia ambapo klabu ya Simba walionekana kuutawala mchezo karibu dakika zote japo wapinzani wao klabu ya Leopards walionekana kukumbuka shuka wakati kumekucha baada ya kuanza kumiliki mpira dakika 15 za mwishoni, hata hivyo mbinu zao hazikufanikiwa na mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho, ubao ulikuwa unasomeka Simba 4-0 AFC Leopards.

Ligi kuu ya Tanzania bara inaanza rasmi tarehe 20 ya mwezi huu na klabu  ya Simba itaanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya klabu ya Ndanda ya Mtwara.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top