Hatimaye Iceland wameyaaga mashindano – Ufaransa waipa kipigo cha rekodi Euro 2016.

Na Charles Kunji
Baada ya kuwaondoa kwenye michuano ya Euro waingereza katika hatua ya 16
bora wiki iliyopita hatimaye kundi la vijana wa 23 kutoka nchi iliyozungukwa na
mabarafu Iceland leo wamerejea nyumbani baada ya kukubali kipigo kizito kutoka
kwa wenyeji Ufaransa cha 5-2.
Iceland walijikuta wakienda mapumziko nyuma kwa magoli 4-0 na
kuweka rekodi ya kuwa timu iliyofungwa magoli mengi zaidi kabla ya mapumziko
kwenye michuano hii ya Euro 2016. Magoli manne yaliyomaliza matumaini mapema
kipindi cha kwanza yalianza kumiminika dakika ya 12. Olivier Giroud ndiye
mfungua nyavu. Dakika chache tu baadae katika dakika ya 19 wafaransa
walishindilia la pili kutoka kwa Paul Pogba. Dimitri Payet akapachika lingine
dakika ya 42 kabla ya Antoine Griezman hajaweka la 4 katika dakika ya 45.

Hata hivyo Iceland walionekana kupata uhai kipindi cha pili wakajipatia
bao la kwanza la kufutia machozi dakika ya 56 kupitia kwa Kolbeinn
Sigtthorsson. Halikudumu sana kwani dakika tatu baadae, Olivier Giroud
alipachika la 5 na kufunga vitabu vya mahesabu kwa upande wa Ufaransa, Kisha
Iceland wakajipatia goli la pili la kufutia machozi katika dakika ya 84 kupitia
kwa Birkir Bjarnason na mpaka mwamuzi anapuliza kipenga Iceland walikuwa
wameyaaga mashindano kwa kipigo kizito zaidi kwenye mashindano haya.

Mchezaji wa kimataifa anayekipiga katika klabu ya Asernal The gunners, Olivie Giroud ndiye aliyeibuka nyota wa mchezo baada ya kupachika wavuni magoli mawili na hivyo kufikisha jumla ya magoli matatu akiwa nyuma ya greezman aliye na magoli manne.

Kwa matokeo haya Ufaransa sasa wataumana na Ujerumani siku ya Alhamisi
kugombania nafasi ya kwenda fainali – Iceland nao wameyaaga mashindano
huku wakiendeleza rekodi ya kuwa timu imefunga goli katika kila mechi ya Euro
mwaka huu.
Na tafsiri halisi ya the game is my fair ukajidhirisha kwa vijana wa
Iceland waliokuwa hawapewi nafasi ya kufanya vyema katika mashindano hayo baada
ya mechi yao kuisha wakakusanyika wote kwa pamoja na kupiga picha kadhaa za
ukumbusho lakini pia wakiwapungia mkono wa kwaheri mashabiki wao wa Iceland.
Post a Comment