SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Jose Mourinho akitambulishwa katika viunga vya CALINTON
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
YASIKIE MANENO YA KOCHA MKUU WA MANCHESTER UNITED WAKATI AKITAMBULISHWA RASMI KLABUNI HAPO. Na charles Kunji. Kocha mkuu wa klab...
YASIKIE MANENO YA KOCHA MKUU WA MANCHESTER UNITED WAKATI AKITAMBULISHWA RASMI KLABUNI HAPO.





Na charles Kunji.




Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Jose Morinho, ametambulishwa leo kuwa kocha rasmi wa mashetani wekundu siku ya jumanne na akisisitiza ya kuwa alikuwa ni mshindi kuamua kuirudisha klabu hiyo katika zama zake za kale.
Morinho mwenye umri wa miaka 53 raia wa ureno aliyebahatika kuvifundisha vilabu vya chelsea, real madrid, pamoja na Inter milan, amesema kuwa hahitaji kuona wachezaji wake wakiimarika wakiwa katika nafasi ya tano mwishoni mwa msimu kama ni kitu chema.
'kwa mashabiki wa United, kwa miaka mingi, mafanikio yalikuwa ni sehemu ya maisha yenu. Katika miaka mitatu iliyopita, ninahitaji msahau" morinho aliwaambia waandishi wa habari.
'Sihitaji kuona wachezaji wakifikiri tunahitaji kufanya vyema.  Kwani nini maana ya kufanya vyema? Kumaliza msimu ukiwa nafasi ya nne? Kwetu sisi kumaliza nafasi ya nne sio malengo yetu, Malengo yetu ni kushinda taji" 
'Nataka kila kitu, nataka kushinda mechi zangu zote, ninataka kucheza vizuri, nataka kushinda magoli, sitaki kuruhusu magoli, ninataka kila kitu" Morinho alifafanua.
Mchezo wa kwanza wa klabu ya Manchester United wakiwa chini ya utawala wa Jose Morinho, utakuwa ni mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Borrusia Dotimund katika kombe la binwa wa kimataifa litakalofanyika katika uwanja wa Shanghai Julai 22. Mechi yao ya kufungua pazia ya ligi kuu ya uingereza itakuwa dhidi ya klabu ya Bournamouth siku ya jumamosi tarehe 13 mwezi agosti.






About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top