
Mabingwa wa kombe la dunia timu ya taifa ya Ujerumani
imekubali kichapo cha goli 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa ambao ni
wenyeji wa michuano ya mataifa ya ulaya mwaka huu.
Huu ulikuwa ni mchezo wa nusu fainali ya pili wakati nusu
fainali ya kwanza ikifanyika hapo jana na kushuhudia timu ya ureno iliyoanza
kwa kususasua kuibuka na ushindi wa goli 2-0 na kujihakikishia nafasi ya
kucheza hatua ya fainali itakayochezwa siku ya jumapili hapo nchini ufaransa.
Pamoja na Ujerumani kuwa na kikosi bora walipoifunga timu ya
Argentina mwaka 2014 katika fainali ya kombe la dunia, bado hawakuweza kufanya
kitu mbele ya wenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya ufaransa na hivyo
ufaransa kuweza kulipa kisasi cha kufungwa na ujerumani katika hatua ya nusu
fainali ya kombe la dunia lililofanyika huko nchini Brazil kwa gali 1-0.
Magoli ya ufaransa yaliwekwa kimyani na mshambuliaji wa
kimataifa anayecheza katika klabu ya Atletical Madrid ya nchini Hispani
akifunga goli la kwanza dakika ya 45+ kwa mkwaju wa penati na akikamilisha
ushindi wa ufaransa dakika ya 72 na hivyo kuwatoa nje timu ya ujerumani waliokuwa
wanapewa nafasi ya kutwaa kombe hilo.
Didier Deschamps ameendelea kumwamini Samwel Umtiti huku akimwacha
nje beki wa kati anayekipiga katika klabu ya Sevilla Ardi Rami lakini pia
kumwacha nje Ngoli Kante na kuwaanzisha viungo Paul Pogba pamoja na Bles
Matuidi walioonyesha kuelewana sana katika idara ya kiungo.
Kihistoria katika mashindano makubwa kama haya ufaransa
alikuwa hana matokeo mazuri sana lakini kwa ushindi huu, Ufaransa anapunguza
lile gap alilokuwa amefungwa na ujerumani.
Fainali ya michuano hii itafanyika siku ya jumapili katika
uwanja wa stade de massele ambapo wenyeji ufaransa watamenyana vilivyo na ureno
timu iliyofika hatua ya fainali ikiwa kama best loser.
Post a Comment