
Jana Pep
Guardiola amenza rasmi kuonja ladha ya kusimama katika benchi la Manchester
City kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Bayern Munich. Namna alivyokuwa akitoa
viashrio vyake unaona kabisa kuna habari mpya. Alikuwa akirusha mikono mara
nyingi tofauti na alivyozoeleka mara nyingi kuweka mikono mfukoni. Uso wake
mara nyingi ulikuwa hauja-relax kama ambavyo imezoeleka. Muda wote alionekana
si mwenye utulivu bali kutoa maelekeza kwa wachezaji wake.
Ni wazi kwamba, lazima haya yangetokea kwenye mchezo wa
kwanza kabisa Guardiola akiwa kocha wa Manchester City. Hata kama ulikuwa ni
mchezo wa kirafiki dhidi ya waajiri wake wa zamani, lakini Guardiola ni kocha
ambaye anapenda kusimamia sana falsafa yake ambayo ni kucheza soka la pasi
nyingi. Ikumbukwe kwamba alikuwa akichezesha vijana ambao hawako ‘familiar’ na
mfumo wake na kubwa zaidi bado hajakaa nao kwa muda mrefu.

Kama uliangalia vizuri mchezo wa jana, basi uliona
tofauti kubwa sana kati ya Guardiola na Ancelotti. Mara nyingi Ancelotti
alionekana kutulia hakuwa na mchecheto. Lakini Guardiola alionekana ni mwenye
mizuka mingi na mara kadhaa alivuka mstari wa eneo lake la kujidai na
kusababisha mwamauzi wa akiba kumrudisha. Unajua kwanini? Bado vijana wake
hawajaupata vizuri mfumo wake.
Licha ya kwamba hiyo ni haiba ya Guardiola, lakini
kikubwa zaidi ni kwamba anahitaji kupandikiza mfumo wake kwenye timu yake hiyo
tofauti na Ancelotti ambaye alikuwa anatafuta namna mpya tu ya kutengeneza
nafasi na sio kutengeneza mfumo.
Baada ya mchezo wa kumalizika na kuelekea kwenye chumba
cha mkutano na wanahabari, Ancelotti aliulizwa maswali juu ya mchezo huo na
kusema kwamba mechi ile inaweza kujirudia kwenye fainali ya Uefa mwakani,
lakini kwa upande wake Guardiola akakataa kabisa. Unajua kwanini? Kwa sababu
ana kibarua kikubwa cha kufanya.
Alisema: “Kwa upande wa Manchester City, mwaka jana
ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
Hawajawahi kufika fainali hata mara moja, hivyo basi historia yetu kama klabu
haifanani kabisa na historia tuliyonayo kwenye Michuano ya Uefa.
“Lazima niwe muwazi. Mimi sidhani kama tunaweza kufika
huko kote. Hakuna shaka kwamba tutajaribu kucheza kwa kadri tuwezavyo, kila
baada ya mchezo mmoja tujitahidi kuimarika. Tutajaribu kufanya hivyo. Lakini
kwa sasa, hatupo hata kwenye Ligi ya Mabingwa. Kilichopo hapa ni kujaribu
kwanza kufuzu halafu mengine yatafuata.”
Mchezo wa jana ulikuwa mgumu kidogo kwake kutokana na
kuwakosa wachezaji muhimu katika kikosi chake kama Sergio Aguero na Kevin De
Bruyne ambao bado wako mapumziko baada ya kumaliza kuzitumikia timu zao za
taifa kwenye Michuano ya Copa America Centenario na Euro 2016
mtawalia. Vincent Kompany na kiungo mpya Ilkay Gundogan bado wako nje
wakiuguza majeraha yao.
Ukosefu wa nyota hao ulitumiwa kwa usahihi na Bayern ambao
walikuwa na nyota wake kama Franck Ribéry, Javi MartÃnez, Xabi Alonso, Philipp
Lahm na David Alaba wote wakiwa kwenye kikosi kilichoanza jana. Kabla ya
kutolewa wakati wa mapumziko, Ribery hasa-hasa alionekana kuinyanyasa sana safu
ya ulinzi ya City ambayo ilikuwa chini ya Aleksandar Kolarov ambaye asili yake
ni beki wa kushoto.
Baadaye Kolarov alitolewa na kuingia Gael Clichy ambaye
pia si nafasi ya beki wa kati si asili yake. Na Guardiola alipoulizwa kama
utakuwa ndiyo mfumo wake alikata na kusema kwamba hiyo ni muda mfupi tu.
“Kolarov yuko imara kwa mipira ya juu, ni mchezaji mwenye
kasi, ana uwezo mkubwa wa kutengeneza mashambulizi kutokea nyuma. Lakini ni
beki wa pembeni,” alisema. Kwa sasa kwenye timu hatua beki yeyote wa kati..wote
ama wako kwenye mapumziko au wanauguza majeraha. Na ndio maana tumemchezesha
Clichy kama beki wakati pia. Hatukuwa na suluhisho juu ya hili kwa leo.”
Pengine wengine watakuja zaidi siku zijazo. City bado
wanahusishwa na usajili wa beki kisiki wa Juventus Leornado Bonucci, licha
kwamba Mabingwa hao wa Italia wanaonekana kuweka kizingiti cha kumzuia beki
huyo kuondoka. Pia kuna tetesi za kumchukua John Stones kutoka Everton.
mchezo wa jana ulikuwa mahususi kabisa kwa Guardiola kukifanyia tathmini
kikosi chake kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi.
Kulikuwa na viashirio vizuri kutoka kwa kinda kutoka
Ukraine Oleksandr Zinchenko ambaye alionesha kuwa mwepesi na mjanja kutokea pembeni
mwa uwanja, bila kusahau Angelino kutoka Uhispania ambaye allicheza vizuri sana
katika nafasi ya beki wa kushoto kabla ya kuhamishiwa kucheza kama winga
baadaye. Wachezaji wote hao ndio kwanza wana miaka 19.
Licha ya kutopata nafasi kubwa msimu uliopita, kipa
Caballero anaweza kufikiriwa upya na Gurdiola kutoka na kiwango chake
alichokionesha jana bila kusahau kipa mwingine kinda aliyeingia kuchukua nafasi
yake Angus Gunn ambaye kwa bahati mbaya aliruhu gaoli pekee katika mchezo
wa jana.
Mbali na hayo yote Guardiola hatasahau mambo mazuri
aliyokuta kwa Bayern ambao ndio waajiri wake wa zamani baada ya kumkaribisha
kwa bashasha huku wakiweka bango kwenye eneo la kuingia kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo lililokuwa limeandikwa “Welcome Back.” ambapo pia
kulikuwa na picha yake.
Mashabiki wa Manchester City watakuwa na furaha baada ya
kuanza kuona mabadiliko kidogo kwenye timu yao ambayo wanahisi utakuwa na
mwanzo mzuri wa mafanikio ya timu yao licha ya kupoteza mchezo wa jana.
Chemistry ya timu ilionekana, wachezaji walikuwa hawauogopi mpira.
Hawapaswi kifukiri mafanikio ya moja kwa moja kwa haraka,
lakini wanapaswa kusubiri Gaurdiola apandikize mbegu zake kwenye timu kisha
kuanza kula mataunda ya mafanikio baada ya muda. Guardiola ni kocha mzuri, hilo
halina shaka na akipewa muda City watafurahia maisha kwenye mchezo wa soka.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete