
USIKU wa January 21 2017 wawakilishi pekee
wa ukanda wa Afrika Mashariki katika michuano ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017, timu ya taifa ya Uganda ilitolewa rasmi katika michuano ya mataifa ya
Afrika yanayoendelea nchini nchini Gabon.
Uganda wameaga mashindano hayo baada ya
kukubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya mabingwa mara 7 wa kombe hilo, timu ya
taifa ya Misri
katika mchezo wao wa pili wa Kundi D.
Uganda wanaaga mashindano hayo na kuwa
wanasubiria mchezo wao wa kukamilisha ratiba dhidi ya Mali, ukiwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba ambapo hata
wakishinda bado hawataweza kufuzu kuendelea na michuano hiyo
Abdallah El Said wa Misri ndio alihitimisha safari ya Uganda katika
michuano ya AFCON
2017, baada ya kufunga goli dakika ya 89 kwa kutumia vyema
assist iliyotolewa na Mohamed Salah.
Hata
hivyo kulingana na rekodi za kwenye makabrasha, Uganda ni timu dhaifu mbele ya Misri, kwani leo wanakuwa wamefungwa kwa mara ya 16 na
mara ya mwisho Uganda kuifunga Misri ilikuwa 1965 katika michuano ya kama hiyo.
Post a Comment