
TIMU ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, maarufu kwa jina la Serengeti Boys inatarajia kuweka kambi nje ya nchi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Congo kwa ajili ya kuwania tiketi ya fainali za mataifa ya Africa.
Katika mchezo wa awali uliopigwa juzi jumapili kwenye dimba la taifa, vijana hao wa kitanzania waliibuka na ushindi wa bao 3-2 yaliyowekwa kimiani na Yohana Mkomola na Abdi mkamba wakati magoli ya Congo yakiwea nyavuni na Langa-lesse na Makouana Beni.
Akithibithisha hayo, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema wanatafuta nchi yenye hali ya hewa sawa na Congo ambayo itakuwa tulivu kwa ajili ya vijana kujiandaa vizuri.
Vijana hao wanatarajia kuondoka siku ya Alhamisi na nchi watakayokwenda bado haijawekwa hadharani.
Mchezo wa marudiano utapigwa tarehe 2 ya mwezi October na mshindi wa jumla atakuwa amefuzu moja kwa moja kucheza fainali za mataifa ya Africa kwa vijana ya mwakani nchini Madagascar.
Post a Comment