Paul Pogba, anakabiliwa na maamuzi
magumu ama ajiunge na MU au la.

Aliyekuwa kiungo mkabaji na nahohadha wa klabu ya Juventus Alessandro
Del Piero, amekubali ya kuwa Paul Pogba anakabiliwa na wakati mgumu juu ya
maamuzi ya kuirudia tena klabu yake ya zamani Manchester United katika rekodi
ya dunia ya paun 100m.
Pogba ambae anakabiliwa na mchezo wa fainali ya euro 2016
dhidi ya Ureno siku ya jumapili, aliondoka katika klabu ya Manchester kwa
uhamisho huru, atarudi klabuni hapo kwa mshahara wa paund 300,000 kwa wiki?
Kwa sasa bado anamkataba na mabingwa wa Seri A, ambao
unamweka klabuni hapo mpaka msimu wa 2019, na Del Piero anaamini vibibi vya
Torino vitaendelea kumtumia kwa mwaka mmoja Zaidi.
‘‘Pogba ni mchezaji mkubwa, ana umuhimu mkubwa sana na tayari
amekwisha onyesha kwa kila mtu,” Alisema Del Piero wakati akihojiwa na sky
sport.
‘‘Sijui kinachokwenda kutokea, mazungumzo yamekuwa ni mengi
mno, lakini nafikiri Juve wanahitaji kumtumia pogba angalau hata kwa mwaka
mmoja, Lakini kwa bahati mbaya United ni klabu kubwa sana, lakini pia ni ngumu
kwa yeye kuchagua wapi ni mahala sahihi kwake. Nikiwa kama Mwitaliano na
mchezaji wa zamani wa Juve, natamani aendelee kuichezea Juve angalau hata mwaka
mmoja Zaidi” Alimalizia Del Piero.
Lakini kiukweli maamuzi yote yapo kwa Pogba ni wapi atataka
kwenda kucheza mpira wake akiwa bado kijana na ukiachilia mbali klabu ya
Manchester United, pia Pogba anafukuziwa kwa ukaribu na Real Madrid ya nchini
Hispania pamoja na mabingwa wa ligi kuu ya ufaransa Klabu ya PSG..
Post a Comment