
Nahodha wa timu ya taifa ya England amesema, shirikisho la mpira nchini England FA limefanya uamuzi sahihi kumteua Sam Allardyce kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Sam Allardyce, 61 maarufu kama Big Sam, ametia kandarasi na shirikisho la mpira la FA kwa miaka miwili akiwa kama kocha wa England, baada ya shirikisho hilo kumalizana na klabu ya Sunderland iliyokuwa bado ina mkataba na meneja huyo.a
Mchezaji shambulizi wa klabu ya Manchester United, na mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya England alikuwa sehemu ya kikosi kilichotupwa nje ya mashindano ya EURO yaliyofanyika huko Ufaransa kwa jumla ya goli 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Iceland katika hatua ya 16 bora.
''Anaweza akaleta mfumo tofauti wa uchezaji katika kikosi chetu" Alisema Rooney. ''Bila shaka ni njia sahihi na tunaweza kufanikiwa tukiwa chini yake" Alieleza Rooney.
Rooney 30, amesema bado hana ndoto za kustaafu soka kimataifa, ''Bado ninaendelea kuwa sehemu ya kikosi cha England" Alisema Rooney aliyeifungia timu yake ya taifa magoli 53 katika mechi 115 alizocheza.''Niliulizwa sana baada ya mashindano ya EURO, lakini ndio, bado nitaendelea kuwepo" Alisema Rooney.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Everton aliyasema hayo akiwa nchini China ambako ndio klabu yake imeweka kambi huko kwaajili ya kujiandaa na msimu wa ligi wa 2016-2017 ambapo huko wameanza na kipigo toka klabu ya Borusia Dortmundi kwa ushindi mujarabu wa magoli 4-1.
Post a Comment