
Sam Allardyce ametangazwa rasmi kuwa meneja mpya wa timu ya taifa ya England.
Allardyce, ajulikanaye sana kama Big Sam, ametia saini mkataba wa miaka miwili, ambao utampatia jukumu la kuandaa na kuongoza timu hiyo hadi mwisho wa Kombe la Dunia la 2018.
Anamrithi Roy Hodgson, aliyejiuzulu baada ya England kuondolewa kutoka kwa michuano ya ubingwa Ulaya nchiniUfaransa baada ya kushindwa na Iceland.
Akiongea na waandiishi wa habari, Big Sam amesema amefurahishwa sana na uongozi wa FA kumuona yeye anafaa kuiongoza timu ya taifa ya ENGLAND na ameweza kuahidi makubwa lakini kuwatia moyo wadau na washabiki wa timu ya taifa ya England ya kuwa amekuja kuwapa neema na si vinginevyo.
'Nimefurahi sana kwani nimekuwa naitafuta kazi kama hii kwa muda sasa, naamini nitafanya vyema" Alisema Big Sam.
Post a Comment