SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Msitoke Bure Yanga, Hata Uzoefu utawafaa sana.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu nyingi za Africa ya Mashariki zimekuwa hazina matokeo mazuri mbele ya timu kongwe katika mashindano mbalimbali kama vile kombe l...


Timu nyingi za Africa ya Mashariki zimekuwa hazina matokeo mazuri mbele ya timu kongwe katika mashindano mbalimbali kama vile kombe la klabu bingwa barabi afrika, shirikisho lakini pia hata katika anga za kimataifa, licha ya timu ya taifa ya Uganda, Uganda the Clames, kuendelea kujikongoja katika hatua ya kutafuta tiketi ya kushiriki kombe la mataifa ya Afrika ya mwakani, timu zote za ukanda wa mashariki, ndoto zao za kufuzu michuano hiyo, zimekwisha yeyuka zamani.
Leo, tuangazie katika ngazi ya vilabu na haswa Zaidi, tutaangalia nafasi ya klabu ya Young African katika mashindano ya shirikisho yanayoendelea. Klabu ya Yanga kufuzu katika hatua ya makundi yaani robo fainali ya kombe la shirikisho barani Africa, ilikuwa ni mwaka 1998 mwaka ambao pamoja na kufuzu katika hatua ya makundi, bado Yanga hawakuweza kufanya vyema.
Katika michezo yote sita ya hatua ya makundi mwaka 1998 yanga aliambulia pointi mbili pekee baada ya kutoa sare mbili na kuweza kufungwa mechi zote nne.
Pengine ya kale yamepita, tuyaache na tugange yajayo. Hivi huu msemo una maana yeyote? Kama ya kale yamepita, na yale makosa tuliyoyafanya hatujifunzi ili tuje na kitu kipya? Mimi kwangu yakale huwa yanasehemu yake katika kunitia moyo, kama nilikosea mahala, nitafahamu wapi nilipokosea ili niweze kurekebisha, na kama nilifanya vyema nitatia juhudi ili nifanye vyema Zaidi.
Turudi kwenye mada yetu, Klabu ya Yanga pamoja na kwamba ilihitaji makubwa tangu walivyopata nafasi ya kucheza katika hatua ya makundi, bado mimi niliona si maana sana kwetu watanzania kujivunia nafasi, bali kwangu ilikuwa ni sehemu ya kupata uzoefu ili, endapo tena Yanga wakajihakikishia nafasi ya kucheza tena katika msimu unaokuja, basi mashindano ya mwaka huu yangekuwa kama Platform katika kuhakikishisha wanatengeneza misingi bora ya kufanya vyema.
Katika mechi tatu Yanga walizocheza wakiwa kundi A, wameweza kupoteza mechi zao mbili kwa klabu ya MO Bejaia kwa goli moja na kukubali kichapo kingine cha goli moja dhidi ya klabu ya TP Mazembe na kuweza kusuruhu na klabu ya Medeama ya nchini Ghana.


Klabu ya Yanga inaburuza mkia kwa pointi moja, huku nafasi ya tatu ikikaliwa na klabu ya Medeama ya nchini Ghana wakati nafasi ya pili ikikaliwa na klabu ya MO Bejaia huku TP Mazembe wakioongoza kundi hilo wakiwa na pointi saba kibindoni.
Katika michezo mitatu aliyocheza yanga, miwili amecheza akiwa katika uwanja wa nyumbani na mchezo mmoja akiwa ugenini huku raundi ya pili akitaraia kusafiri kuwafuata Medeama, na TP Maezembe na kusaliwa na mchezo mmoja hapa nyumbani.
Ni vigumu sana kupata matokeo katika viwanja vya ugenini hasa kwa Kariba ya vilabu anavyocheza navyo Yanga. Uongozi wa klabu ya Yanga walikosea kuwekeza nguvu nyingi kwa mashabiki ya kuwa wanakwenda kufanya vyema wakati walikuwa wanajua kwa nadharia aina ya timu walizokuwa wamepangwa nazo, huku kivitendo hatukuweza kukubali matokeo.
Na ndio maana hata ile kauli yangu ya kuwaasa mashabiki kutokupandikiza akili ya ushindi kisha Yanga wakifanya vibaya, waonekane hawajui. Kwangu mimi huu ni uzoefu wa hali ya juu ambao klabu ya Yanga wameupata kwa mwaka huu.Wana kazi kubwa sana ya kuhakikishwa kile walichokuwa wanakiita ‘‘Tuna uhakika tunakwenda kushinda, wakakifanya katika mashindano yajayo.”

Kwangu mimi naiita, Yanga walikwenda kushiriki kupata uzoefu, na ndio maana hata sishitushwi na matokeo wayapatayo sasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top