boy
boys boys
Timu ya soka ya taifa
ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' jana Mei 19, 2016
imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea
Kusini katika mfululizo wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na
Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16). Katika mchezo huo
uliofanyika uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India, mabao ya Serengeti
yalifungwa na Assad Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya
87 ambaye alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1. Matokeo hayo
yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri matokeo ya
mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa timu itakayocheza
fainali. Serengeti Boys watashuka dimbani tena dhidi ya Malaysia Mei 21, 2016. Fainali
ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016 na kabla ya mchezo wa fainali,
utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco,
Goa nchini India. India imeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka
17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya fainali za kombe
la dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.
TFF wana kazi kubwa ya
kuhakikisha ubora wa hawa watoto haupotei na ili siku moja waje kupandishwa
katika timu kybwa ya taifa [taifa stars]
Lakini watoto hawa
wakiishia mitaani na wakakosa cha kufanya miaka ijayo itakuwa ni sawa na taifa
kufanya kazi bure.7
By Kunji, Charles.
Post a Comment