SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Huenda ukawa msamaha wa VAN GAAL.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Manchester United washinda Kombe la FA Image copyright GETTY Image caption Jesse Lingard alifungia United bao la ushindi Manchester ...

Manchester United washinda Kombe la FA



Jesse LingardImage copyrightGETTY
Image captionJesse Lingard alifungia United bao la ushindi

Manchester United wameshinda Kombe la FA baada ya kuwalaza Crystal Palace 2-1 katika fainali iliyochezewa uwanja wa Wembley.
Ni mara yao ya kwanza kushinda kikombe hicho tangu 2004.
Mabao ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata katika dakika ya 81 na Jesse Lingard.aliyefunga goli hilo la ushindi katika dakika ya 110
Bao la kufutia machozi la Crystal Palace limefungwa na Jason Puncheon.katika dakika ya 78
Ushindi huo ni nafuu sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutokana na kutofanya vizuri  kwa klabu hiyo.
Kwa ushindi huo, Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Van Gaal alisema amefurahia sana kushinda kikombe hicho.
"Ni muhimu sana kushindia klabu kikombe hiki, kwa mashabiki, na mimi pia kwa sababu sasa nimeshinda katika mataifa manne, na si mameneja wengi wamefanikiwa kufanya hivyo," amesema.
"Tukiwa na wachezaji 10, na tulikuwa tumecheza Jumanne jioni pia, lakini tulistahiki. Lilikuwa bao zuri sana, sio?"

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top