SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: JOSEPH OMOG AJIHAMI NA VIWANJA VYA MIKOANI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
picha na saleh jembe. KOCHA wa klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba, Joseph Omog amesema kikosi chake ni lazima kifanyiwe mabadiliko kue...
picha na saleh jembe.

KOCHA wa klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba, Joseph Omog amesema kikosi chake ni lazima kifanyiwe mabadiliko kuelekea kwenye michezo ya nje ya mji wa Dar es salaam.

Omog amefafanua kuwa, viwanja vya mikoani vina changamoto kubwa sana hivyo ni lazima wafanye baadhi ya mabadiliko ya kikosi ili kuisaidia timu iweze kupata matokeo kwenye viwanja vya mikoani.

"Sio mabadiliko makubwa, bali ni mambo ya kiufundi tu, ili tuweze kuendeleza sera yetu ya kushinda kila mechi inayokuja mbele yetu" Alisema Omog.

Mechi ya kwanza Simba kuanza kutupa karata yake nje ya DAR ES SALAAM ni dhidi ya timu ya  Mbeya City, mchezo utakaopigwa siku ya jumatano kwenye dimba la Sokoine.

Hata hivyo, Simba imethibitisha ya kuwa itaondoka mapema kuelekea Mbeya ili ikiwa njiani ipate mchezo mmoja wa kujipima nguvu na timu yeyote mjini Iringa.

Tayari Simba imekwisha cheza mechi saba, tano kati ya hizo ikiibuka na ushindi na kutoka sare mechi mbili na kujikusanyia jumla ya pointi 17 na hivyo kukaa kileleni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top