
WADHAMINI wa ligi kuu Tanzania bara, VPL, kampuni ya simu ya Vodacom imesikia kilio cha mashabiki wa mpira wa miguu nchini na duniani kote na kuja na suluhisho la kukata kiu hiyo ya mshabiki kwa kuanzisha kifurushi cha vodacom kikijulikana kwa jina la SOKA BANDLE.
Kifurushi hicho ambacho ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mpira wa miguu, kitawapatia mashabiki hao dakika 14 za vodacom pamoja na dakika mbili a mitandao yote pamoja na SMS 20 kwa masaa 24.
Kifurushi hicho chenye thamani ya shilingi 500 kitawawezesha mashabiki wa mpira wa miguu nchini na duniani kote kuwasiliana kwa ajili ya kupata updates za soka hapa nchini na duniani kote.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasilianoi wa kampuni hiyo Nandi Mwiyombella amesema, “Kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-mashabiki wa soka wanaotumia mtandao wa Vodacom watapata taarifa mbalimbali za soka za hapa nyumbani na kimataifa kwa kipindi cha siku 7,dakika 14 za muda wa maongezi Vodacom kwenda Vodacom, dakika 2 za muda wa maongezi kwa mitandao yote na jumbe fupi za maneno (SMS) 20 kwa kipindi cha masaa 24”
Alisema Vodacom Tanzania imeleta kifurushi hiki cha ‘Soka bando’ kipindi hiki ambacho msimu wa ligi ya VPL unaendelea ni furaha kwa Mtandao wa Vodacom kuwawezesha mashabiki kupata taarifa za ligi kwa urahisi kupitia mtandao wake ikiwemo kuwapatia burudani wateja wake na watanzania wote kwa ujumla.
“Kampuni inathamini na kutambua mchango wa mashabiki katika kukuza ligi hii tangu ilipoanza kuidhamini hivyo ndio maana tumewaletea kifurushi hiki ili wapate burudani na taarifa za soka kwa wakati na kwa gharama nafuu”.Alisema Mwiyombella.
Ili kununua kifurushi hiki anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga namba *149 * 01#, na kuchagua ‘Soka Bando’. Baada ya hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga” “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460. Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya Mspoti.vodacom.co.tz.
Wateja watakaojiunga na huduma hii pia watapata nafasi ya kufurahia ofa na zawadi mbalimbali kutoka Vodacom kama vile muda wa bure wa maongezi, sms au MB za kuperuzi inteneti hususani timu wanazoshabikia zitakapokuwa zimeibuka na ushindi wa mchezo.
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya VodacomTanzania bara unaendelea katika viwanja mbalimbali nchini.
shida ya Manchester sio kwa mchezaji mmoja mmoja, Bali no timu kwa ujumla.
ReplyDelete