SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: MAN UNITED YAENDELEZA MATOKEO MABAYA CHINI YA MOURINHO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya Manchester United chini ya mkufunzi, Jose Mourinho imepokea kipigo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushuhudia ikifungwa mabao...
TIMU ya Manchester United chini ya mkufunzi, Jose Mourinho imepokea kipigo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushuhudia ikifungwa mabao 3-1 dhidi ya Watford, mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye dimba la Vicarage Road, uwanja unaotumiwa na klabu ya Wartford kama uwanja wa nyumbani.
Watford walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 34 lililofungwa na kiungo mshambuliaji wao Etienne Capoue lililoduma mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku klabu ya ManUnited ikitafuta nafasi ya kusawazisha na Dakika ya 62 mshambuliaji kinda wa Man United Marcus Rashford alisawazisha bao hilo baada ya mabeki wa Watford kushindwa kuokoa kichwa alichopiga na mpira kumrudia tena na kuukwamisha mpira wavuni.

Waford walipata bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wao aliyetokea benchi Juan Camilo Zuniga mnamo dakika ya 84 na kuwachanganya kabisa United.
Wakiwa bado wanajiuliza namna gani ya kusawazisha na pengine kuongeza bao, United walijikuta wakiruhusu bao la tatu lililofungwa na Troy Deeney kwa mkwaju wa penati dakika ya 90 baada ya Fellaini kumchezea madhambi Zuniga.
Hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa Mourinho kupoteza michezo mitatu mfululizo ya ligi kwenye msimu tangu ilivyotokea Februari 2002, wakati huo akiwa meneja wa Porto.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top