KOZI
maalumu
ya ukocha wa soka la wanawake imefikia tamati leo katika makao makuu ya
shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.
Kozi hiyo iliyoanza
siku ya jumatatu, ilikuwa na lengo la kuinua soka la wanawake nchini ambalo
linaonekana kutokuwa sawa tangu awali.
Akifunga kozi hiyo
katibu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF, Selestin Mwesigwa amesema
makocha waliopata fursa ya kujifunza kozi hiyo wakaitumie ili kuinua soka la
wamawake nchini.
“Tumewagharimia ili mje
kusaidia soka la wanawake na sio kwenda kutundika vyeti hivi ukutani” Alisema
Mwesigwa.
Aidha, katibu wa TFF
aliongeza kuwa suala la vifaa bado lipo jikoni na hivyo makocha hao wawe na
subra wanapotafutiwa vifaa hivyo kama vile jezi, mipira pamoja na vifaa vingine
lukuki.
“Tunataka kuiomba
serikali itusamehe kodi kwani kuna vifaa vingi ambavyo vipo bandarini na
tunashindwa kuvitoa kwa sababu ya kodi” Alisema.
Lakini pia mkufunzi wa
kozi hiyo Bi Andrea, mwakilishi wa FIFA kutoka Mexico amefurahishwa na kozi
hiyo ambayo imetolewa na shirikisho la mpira la Tanzania kushirikiabna na FIFA.
Post a Comment