SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: CRISTIANO RONALDO KUREJEA UWANJANI BAADA YA MIEZI MIWILI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MSHAMBULIAJI wa kimataifa, Christian Ronaldo anatarajia kuwa uwanjani kwa mara ya kwanza tangu apate majeraha katika michuano ya EURO  ya...
Real Madrid and Portugal forward Cristiano Ronaldo


MSHAMBULIAJI wa kimataifa, Christian Ronaldo anatarajia kuwa uwanjani kwa mara ya kwanza tangu apate majeraha katika michuano ya EURO  yaliyofanyika nchini Ufaransa miezi miwili iliyopita.

Ronaldo ambaye amekosa michezo mitatu ya mashindano yote anatarajia kuwa uwanjani kwenye mechi dhidi ya klabu ya Osasuna wikiendi hii.

Kwa muda wote huo Ronaldo amekuwa anauguliwa jeraha la goti alilolipata alipogongana na mshambuliaji wa Ufaransa Dimitri Payet, kwenye mchezo ambao Ureno iliibuka na ushindi wa goli 1-0.

"Tuna furaha kumwona anarejea tena baada ya muda mrefu kuwa nje ya uwanja" Alisema meneja wa klabu hiyo, Zinedine Zidane.

"Hii ni mechi yake ya kwanza ya msimu tangu akae nje kwa miezi miwili sasa"Alisema .

Ronaldo alishinda magoli 35 katika mechi 36 za Laliga ambapo Real Madrid alimaliza mshindi wa pili nyuma ya klabu ya Barcelona.

Lakini pia Ronaldo alikosa mchezo wa taifa wa kirafiki dhidi ya Gibralter waliposhinda goli 5-0 September mosi na kipigo cha goli 2-0 dhidi ya Switzaland katika mchezo wa awali wa kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini  Russia.

Madrid ambao walishinda dhidi ya Sevilla kwenye kombe la super cup, wameshinda mechi zao mbili za ufunguzi kwenye ligi ya Hispania.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top