Leicester yamsajili Nampalys Mendy


Na Charles Kunji
Katika jitihada za kuhakikisha kikosi chao kinakuwa bora kabla ya kuingia kwenye harakati za kutetea taji lao, Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City wamemsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Nampalys Mendy.
Mchezaji huyo zamani akiichezea klabu ya Nice ametia sahihi kandarasi ya miaka minne kufanya shughuli nchini Uingereza.
Hata hivyo, Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 hajawahi kuitwa katika kikosi cha taifa cha Ufaransa.
Akiongea wakati anakaribishwa klabuni hapo, mendi alisifu ubora wa klabu hiyo lakini pia na mkuu wake wa kazi mpya.
'Namfamu kocha, nafahamu uwezo wake lakini pia nafahamu falsafa yake natumai nitafanya kazi." aliongea hayo Mendy
Mendy alijiunga na Nice mwaka wa 2013 akitokea klabu ya Monaco alikoichezea katika mechi 110 za ligi ya daraja ya juu Ligue 1 katika misimu 3.
Mendy ni mchezaji wa tatu kujiunga na mbweha wa jangwani baada ya kipa Ron-Robert Zielerand na mlinzi Luis Hernandez.
Post a Comment