
N Charles Kunji
Mshambuliaji wa Borussia Dotmund Henrikh Mkhitaryan amekamilisha dili na klabu ya Manchester united kwa uhamisho wa paund mil 26.
Henrikh Mkhitaryan raia wa Armenia ameafikiana na uongozi wa BVB na
kuondoka klabuni hapo baada ya viongozi hao kuona huenda akaondoka kwa usajili
huru baada ya kugoma kuongeza mkataba mwingine.
Afisa mkuu wa
Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema kuwa wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwa
United ili kumzuia nahodha huyo wa Armenia kuwa ajenti huru mwishoni mwa msimu
ujao.
'Iwapo
tungekataa mchezaji huyo angekuwa huru mwaka 2017'' ,Watzke aliambia mtandao wa
Dortmund.
Henrikh Mkhitaryan anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na mashetani
wekundu chini ya morinho ikiwa imewasajili wachezaji wawili msimu huu
akiwemo beki Eric Baily na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
Mkhitayran alijiunga na Dortmund 2013 kutoka klabu
ya Ukrain Shakhtar Donetsk kwa pauni milioni 23.
Post a Comment