Fifa yamtimua naibu katibu

Shirikisho la soka duniani Fifa limemtimua naibu katibu wake Markus Kattner kwa kujihusisha na ukiukwaji wa matumizi ya siri ya mamilioni ya dola.
Kattnet raia wa Ujerumani mwenye
umri wa miaka 45 alikua akiitumikia nafasi hiyo baada ya aliyekua katibu Jerome
Valcke kutimuliwa kazi kutokana na kashfa za rushwa.
Kufutwa kazi kwa kiongozi huyu
kulikuja mara moja baada ya bodi ya uchuguzi ya ndani ya Fifa kugundua kulikua
na ukiukwaji na uvunjaji wa majukumu yake.
Kulikuwa na ushahidi wa kutosha
kuonyesha mapungufu katika majukumu yake kwa kutumia pesa za ziada ambazo
waliamua kiasi gani rais, katibu mkuu na naibu katibu mkuu walipwe.
Post a Comment