
TIMU ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti boys imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya vijana ya Congo katika uwanja wa taifa, jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wa kuwania tiketi ya fainali za mataifa ya Africa za vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika nchini Madagascar, mwakani.
Serengeti Boys ilipata magoli yake kupitia kwa wachezaji, Yohana Mkomola, aliyepachika mabao mawili huku Makamba akimalizia bao la tatu lililopelekea ushindi wa vijana hao.
Congo walifunga bao lao la kwanza kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Lenga-lesse baada ya beki wa Serengeti Boys kumwangusha Mbongo ndani ya Penalty Box.

Hata hivyo, vijana wa Serengeti Boys walipata pigo kwenye kipindi cha pili baada ya kipa wao
tegemezi, Ramadhani Kabwili kupata majeraha alipokuwa akijaribu kuokoa mkwaju wa penalty uliopigwa na Lenga-Lesse.
Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inatakiwa kushinda kwa ushindi wa aina yeyote kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa October 2 nchini Congo.
tegemeo LA timu ya taifa ya kesho lipo kwa vijana hawa. fanyeni jihada tena viongozi ili wapate kambi ya nje
ReplyDelete