MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya England na klabu ya Liverpool Daniel Sturridge alifunguka na kusema kwamba usipotumia nguvu nyingi kwenye mechi unazopata nafasi, basi utakuwa ni mtu wa kukaa benchi kila kukicha kutokana na kuwa na upinzani mkali wa namba kwenye kikosi hicho.
Kila kukicha klabuni hapo kunaongezeka ushindani wa namba na kutokana na kila mtu kutaka kumdhihirishia kocha wa timu hiyo, Klopp ya kwamba anaweza kucheza kwenye kikosi cha kwanza na kuwazidi wachezaji wengine.
Kabla ya mechi ya jana kwenye uwanja wa Anfield dhidi ya timu ya Tottenham, Sturridge alikuwa akikaa benchi lakini jana alipangwa kwenye kikosi cha kwanza na kupachika magoli 2, pale liverpool waliposhinda 2-1 dhidi ya Tottenham.
"Tumekuwa wengi sana tunaogombea namba, hivyo najituma kila kukicha kumdhihirishia kocha na mimi nina kitu cha kuipa klabu yangu" Alisema Sturridge alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha TV baada ya mechi.
"Kila mtu ana kipaji, mtazame Sadio Mane, akina Coutinho Firmino kila mtu ana njaa ya mpira na mimi lazima nishinde ili nijitengenezee namba yangu" Aliongeza Sturridge.
Ushindi huu unaipeleka Liverpool mbele na kusubiri matokeo ya mechi za leo kabla droo nyingine haijapangwa ya kujua nani atakutana na nani.